MRADI WA MWENDOKASI WAWA UTALII

Maafisa kumi na sita kutoka serikali ya Senegal wako nchini kwa ziara ya mafunzo ya namna ya uendeshaji wa mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza kutekeleza mradi kama huo mjini Darkar nchini Senegal.

Mkuu wa msafara wa maafisa hao 16 kutoka Senegal amesema wamekuja Tanzania baada ya kuona mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika uendeshaji wa mradi huo na kwamba wanaamini kupitia Tanzania wataweza kujifunza namna nzuri ya uendeshaji wa BRT ambao wanatarajia kuanzisha mjini Darkar mapema mwaka 2021.

Kaimu mtendaji mkuu wa wakala wa mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam amesema wako katika hatua za mwisho za kumtafuta mwekezaji mwingine atakayefanya kazi na UDART ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa mradi huo huku akisema katika awamu ya pili wanatarajia kusafirisha abiria zaidi ya laki nne kwa siku.

Watumiaji wa mabasi hayo yaendayo haraka wameiambia ITV kuwa tangu mradi huo kuanza umekuwa na manufaa makubwa ambapo sasa usafiri umerahisishwa tofauti na awali huku pia wakitoa rai kwa maafisa wa DAR Tna UDART.

Chanzo: ITV

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

UJUE UMBALI KUTOKA DAR KWENDA MIKOA MBALIMBALI..

RASTAFARI MWENYE NYWELE NDEFU KULIKO WOTE TANZANIA

WATU WEUSI TUNA AKILI NDOGO ???