MATANGAZO YA TV ZETU ZA KIBONGO KUKOSA MPANGILIO

Kweli nakubali kwamba sisi ni masikini sana na ili vyombo vya habari vijiendeshe vinahitaji fedha ambayo inatokana na matangazo,kinachoniudhi na kunikwaza ni pale ambapo unaangalia TV mara linatokea tangazo la sabuni mara 'Revola ni sabuni nzuri' baada ya dakika mbili unaona'Protex hulinda ngozi yako' kidogo tu unaona'Rungu ni sabuni bora' mara geisha mara sijui nini au katika mitandao ya simu ,ohh 'Vodacom inaongoza kidogo tu Celtel imeenea mara kidogo tu 'Tigo viwango nafuu' yaani ndani ya nusu saa matangazo kibao yote yanatangaza huduma moja sasa sisi watazamaji hasa mimi nashindwa kufanya uamuzi kipi bora,mimi nadhani vyombo vya habari vingekuwa na policy kama wanaamua kupromoti Revola au Tigo iwe ni siku nzima kama ili kuepuka kutuchanganyachanganya hivi...

Comments

Popular posts from this blog

UJUE UMBALI KUTOKA DAR KWENDA MIKOA MBALIMBALI..

RASTAFARI MWENYE NYWELE NDEFU KULIKO WOTE TANZANIA

WATU WEUSI TUNA AKILI NDOGO ???