ASKOFU MWINGIRA ADAIWA KUZAA NA MKE WA MTU.

Heshima kwenu wakuu,

Mahakani Kisutu: Askofu wa Makanisa ya Efatha Josephat Mwingira, amekataa katakata kupima DNA ili kutambua mtoto wa Dk. Phillis Nyimbi ambaye ni mke wa Dk. William Morris ni wa nani.

Amedai hawezi kupima DNA wakati mtoto si wake.

Baada ya Usikilizwaji wa kesi hiyo, Askofu Mwingira alipitishwa Mlango wa Nyuma kukwepa Kamera za Waandishi wa habari kinyume na Washitakiwa wengine ambao hupigishwa magoti mbele ya Camera.

Hapa ndo nashindwa kuelewa kwanini Mahakamani wanafanya mambo ya Upendeleo. Wengine Wanaruhusu wapigwe picha wengine wanakataza.

Ijumaa ya tarehe 15Dec 2017, Huyo mwanamke anayedaiwa kuzaa na Mwingira alitoa ushahidi wake. Alisema hajazaa na Mwingira wa Moris, bali alizaa na mfanyabiashara Mwingine tu.

MKE wa Dk. William Morris, Dk. Philis Nyimbi, anayedaiwa kuzaa na Nabii Josephat Mwingira, alikana mahakamani kwamba haujui mwili wa nabii huyo wala hajawahi kuzaa naye.

Anadai aliamua mwenyewe kuzaa mtoto na mfanyabiashara ambaye sasa ni marehemu na kwamba mtoto huyo si wa Nabii Mwingira wala Dk. Morris.

Dk. Nyimbi alitoa utetezi huo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mhini, kwa kuongozwa na Wakili wake, Peter Swai.

Alidai mwaka 2001 alifunga ndoa na Dk. Morris katika Kanisa la Mtakatifu Albano na walikaa mapumziko ya siku tatu katika Hoteli ya Starlight kisha wakahamia Muhimbili alikoishi katika chumba kimoja akiwa kwenye mafunzo ya vitendo.

“Niliishi naye katika chumba kimoja kwa miezi mitatu, aliniahidi tutaenda kuishi Marekani lakini kadiri siku zilivyokuwa zikienda hakukuwa na safari, mwishowe nikaanza kuona aibu kwa madaktari wenzangu, kila wakikaa walikuwa wananiuliza naondoka lini.

“Nilipoona hatuondoki nikaona nimuulize safari yake ina tatizo gani akanieleza kuna tatizo la tiketi, nikamsaidia kumaliza tatizo hilo akafanikiwa kuondoka peke yake Februari, 2002, mimi nikabakia akasema nitamfuata tukaishi huko.

“Mawasiliano yalikuwa ya shida, nilichanganyikiwa sana, madaktari wenzangu walikuwa wakinihoji naondoka lini, nilikuwa nalia tu. Nmelinukuu Gazeti la Mtanzania

My Take:

Kama kweli Askofu hahusiki na kuzalisha Mke wa mtu, kwanini akatae kupima DNA? Mimi napendekeza apime ili kuondoa utata na kujisafisha kwenye Jamii inayomzunguka.

Comments

Popular posts from this blog

UJUE UMBALI KUTOKA DAR KWENDA MIKOA MBALIMBALI..

RASTAFARI MWENYE NYWELE NDEFU KULIKO WOTE TANZANIA

WATU WEUSI TUNA AKILI NDOGO ???